
Kikosi cha KMC kikijinoa kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Sooting
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Afisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema maandalizi ya kuelekea mchezo huo yamekamilika kwa asilimia kubwa na kwamba kikosi hicho kipo tayari kuvaana na wapinzani hao katika soka na hivyo kuleta furaha kwa mashabiki wa timu ya KMC FC.
Katika mchezo huo timu ya KMC FC ambao ni wageni dhidi ya Ruvu Shooting imejiandaa kufanya vizuri na hivyo kurudisha hari waliyokuwa nayo wakati ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2020/2021 ulipoanza Septemba mwaka huu ambapo iliweza kushinda michezo mitatu mfululizo.
Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Kocha Mzawa Habibu Kondo kwakushirikiana na mshauri wa Benchi la ufundi,John Simkoko hadi sasa hakina majeruhi na kwamba wachezaji wote wana Afya nzuri.
KMC FC hadi sasa imecheza michezo sita ambapo kati ya hizo imeshinda michezo mitatu, imepoteza miwili na kutoka sare ya kutokufungana mchezo mmoja ambao ulikuwa dhidi ya Coast Union ya Mkoani Tanga na kuiwezesha kuwa na alama 10 huku ikiwa kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara.