Jurgen Klopp na Mohamed Salah
Mohamed Salah amefunga mabao kadhaa ya penalti msimu huu, huku baadhi ya hizo zikilalamikiwa kuwa anajidondosha ili kuisaidia timu yake kupata matokeo, ikiwemo katika mchezo dhidi ya Newcastle United mwezi uliopita na dhidi ya Crystal Palace mwezi huu.
"Mchezo dhidi ya Crystal Palace ndiyo ambao alidondoka chini bila kupewa penalti, lakini mnazungumzia tuu matukio mengine", amesema Klopp.
"Katika matukio mengine hakukuwa na kitu cha kujadili, ni penalti za uhalisia. Kama hii ndiyo ya kwanza, kwanini inazungumzwa hivyo?. Kuna mazingira mengi kama haya yanatokea kwenye timu zingine lakini hatuyazungumzi kwasababu sio Manchester City, sio Liverpool, sio Manchester United, Arsenal au Chelsea", ameongeza.
Liverpool inakutana na Leicester City Jumatano hii katika Uwanja wake wa nyumbani wa Anfield, ikisaka alama tatu muhimu za kujizatiti kileleni mwa ligi kwa tofauti ya pointi 7 baada ya mpinzani wake wa karibu Manchester City kupoteza mchezo wake wa Jumanne dhidi ya Newcastle United.




