Simba SC yenyewe itaingia uwanjani siku ya Jumamosi ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya FC Bravos ya kutokea Angola kwenye mchezo wa kwanza wa makundi uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.
Klabu za Yanga na Simba zitashuka uwanjani kukipiga ugenini katika michezo ya vilabu Afrika klabu bingwa na shirikisho mwishoni mwa wiki Jumamosi na Jumapili zote zitacheza nchini Algeria.
Kikosi wa Wanajangwani kitacheza na mabingwa wa klabu bingwa Afrika wa mwaka 1976 MC Algers siku ya Jumamosi Disemba 7 wakati Simba SC itakuwa na kibarua kizito siku ya Jumapili Disemba 8 dhidi ya Club Sportif Constantine.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara yenye makao yake makuu Mitaa ya Twiga na Jangwani kitaingia uwanjani siku ya Jumamosi kikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza mchezo wa kwanza wa makundi uliochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam kwa kufungwa magoli 2-0 dhidi ya Al Hilal ya Sudan.
Yanga SC inapitia wakati mgumu msimu huu kutokana na kutokuwa kwenye ubora wake wa misimu miiwili iliyopita kabla ya kupoteza mchezo wa klabu bingwa ilipoteza michezo miwili ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya timu za Azam FC na Tabora United kwa magoli 1-0 na 3-1.
Simba SC yenyewe itaingia uwanjani siku ya Jumamosi ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya FC Bravos ya kutokea Angola kwenye mchezo wa kwanza wa makundi uliochezwa uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es salaam.
Kikosi cha Wekundu wa Msimbazi kinamwendelezo mzuri wa ushindi msimu huu lakini changamoto inakuja namna ya ushindi huo unavyopatikana, Kocha Fadlu Davies bado anahangaika kutafuta kikosi chake cha kwanza timu inacheza vizuri dakika 45 ya kipindi cha kwanza kipindi cha pili huwa kikosi kinapoteza ubora wake.
Timu hiyo yenye makao yake makuu Mtaa wa Msimbazi Kariakoo ikikutana na timu yenye uwezo mzurio wa kuzuia na kushambulia Simba inaweza kujikuta katika wakati mgumu wa kupoteza mchezo mpaka sasa Mwalimu Fadlu bado anajaribu kikosi chake hii inaweza kuwa changamoto kwenye michezo mikubwa ya kombe la shirikisho.
Timu ya Wananchi pia bado inamatatizo kwenye uchezaji wake namna timu hiyo inavyozuia inashida ikicheza dhidi ya timu yenye Washambuliaji wazuri wa kutumia nafasi nayo inaweza kujikuta katika wakati mgumu.
Yanga SC inanolewa na Kocha mpya akiwa hana hata wiki mbili kwenye timu hiyo kuna changamoto wa Wachezaji kuelewa aina ya falsafa yake hii itasabisha Yanga kuadhibiwa dhidi ya Wapinzani wakubwa kombe la klabu bingwa Afrika.
Yanga SC imeondoka leo Alasiri kuelekea nchini Algeria wakati Simba inatarajiwa kuondoka Alfajiri ya kesho Disemba 4 nayo inaelekea Algeria.
Mashabiki wa timu hizo Wamewataka Wachezaji kwenda kujituma na kupambana ili kurudi na matokeo ya ushindi katika michezo hiyo ya ugenini nchini Algeria dhidi ya MC Algers na Club Sportif Constantine.