Ijumaa , 18th Nov , 2022

Kiungo Abdul Suleiman, ‘Sopu’ ameanza kurejea kwenye ubora wake baada ya kuwa nje kwa muda akitibu majeraha yake.

Ingizo hilo jipya kutoka Coastal Union hajawa kwenye mwendo bora ndani ya Azam FC kwa kuwa mudamwingi anatumia akiwa nje ya uwanja.

Kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting wakati Azam FC ikishinda bao 1-0 alionyesha makeke yake kwenye mchezo huo Uwanja wa Azam Complex.

Azam FC ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 26 baada ya kucheza mechi 12 na kufunga mabao 17 ametoa pasi moja ya bao.

Mchezo ujao wa Azam FC ni dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Majaliwa Novemba 20.