
Tuisila Kisinda
Mutuale amesema Kisinda alisajiliwa na Yanga akitokea As Maniema ya Dr Congo ambayo itapata mgawo wa asilimia kadhaa katika fedha itakayopatikana kutokana na mauzo ya Kisinda.
"Watu waelewe Kisinda alikuwa akicheza As Vita kwa mkopo akitokea Fc Manyema, hivyo Yanga walimsajili kutoka As Maniema. Pia Tonombe Mukoko ni mchezaji wa Yanga walimsajili kutoka As Vita, ofa zinazotumwa zote zinaenda Yanga hata Sasa hivi ipo ofa kutoka Tunisia, Yanga wakikubali wao ndio watapokea pesa, hayo maneno mengine ni uzushi mtupu Mimi ndiye meneja wa wachezaji wote hao". amesema Meneja ambae pia ni wakala wa Tuisila Kisinda na Tonombe Mukoko Nestori Mutuale akizungumza na mwandishi wetu David Kampista
Wakala huyo ametoa kauli hiyo kufuatia uwepo wa taarifa kuwa klabu ya Maniema ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo ilikuwa ikimmiliki winga huyo kuwa ndio iliyopokea ofa ya usajili ya Kisinda kutoka katika klabu ya RS Berkane ya Morocco na ripoti hizo zikidai kuwa mchezaji huyo yupo yanga kwa mkopo hivyo Yanga haitafaidika na usajili wa mchezaji huyo.