Jumatano , 30th Nov , 2016

Kipa raia wa Ghana aliyekuwa akiichezea timu ya Medeama Daniel Agyei ametua nchini tayari kumalizana na Simba.

Daniel Agyei

 

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema, Kipa huyo, anatarajia kusajiliwa na Simba baada ya kocha mkuu wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog kutoa mapendekezo hayo kwenye ripoti yake aliyoikabidhi hivi karibuni.

"Agyei amekuja kusaini mkataba wa kuichezea Simba, hiyo yote ni katika kuifanyia kazi ripoti ya kocha wetu aliyoitoa kwa uongozi katika usajili huu wa dirisha dogo," Alisema Manara.

Kutua kwa kipa huyo, kutafanya idadi ya makipa kuongezeka na kuwa wanne ambao ni Manyika Peter Jr, Denis Richard, Vincent Angban na Agyei mwenyewe.