Jumatano , 2nd Sep , 2015

Kikosi cha timu ya Taifa Stars kimewasili nchini hii leo kikitokea nchini Uturuki ambapo kiliweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya kuwania kucheza fainali za AFCON dhidi ya Nigeria itakayopigwa Jumamosi uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika taarifa yake Kocha wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema, wachezaji wote wapo salama isipokuwa mchezaji mmoja Abdi Banda ambaye ni majeruhi na hatokuwepo katika mechi hiyo, huku akiamini juhudi, ushirikiano na uelewa wa wachezaji ndio njia ya ushindi katika mechi hiyo.

Kwa upande wa wapinzani wao kikosi cha timu ya Nigeria Super Eagles kinatarajia kuwasili nchini siku yoyote kuanzia hii leo kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo.