Jumanne , 5th Jul , 2016

Kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serenget Boys kimevunja kambi rasmi leo na kwenda mapumziko ambapo kinatarajia kurejea tena Julai 12 mwaka huu kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Afrika Kusini.

Serengeti Boys wakishangilia moja ya bao la ushindi.

Akitangaza kuvunjwa kwa kambi hiyo kocha mkuu wa kikosi hicho Bakari Shime ametoa wito kwa wadau, makampuni na serikali kuisaidia kwa hali na mali timu hiyo ili ipate maandalizi mazuri yatakayoiwezesha kufuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwakani nchini Madagascar.

Shime ambaye ni muumini wa soka la vijana amesema kama timu hiyo itaungwa mkono moja kwa moja itaweza kuiondosha Afrika Kusini ambayo imekuwa kikwazo kwa Tanzania katika mashindano mbalimbali.

Kwa mujibu wa ratiba ya shirikisho la soka Barani Afrika CAF, Serengeti Boys itaanzia ugenini mnamo Agosti tano, sita au saba kuumana na Afrika Kusini na endapo itavuka kigingi hicho itavaana na mshindi kati ya Congo Brazaville na Namibia katika hatua ya mwisho.