
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela wa kwanza (Kulia) akizungumza na Waandishi wa Habari.
Mwakalebela ametoa kauli hiyo hii leo alipozungumza na Kipenga na kusema kwamba hawashitushwi na kuona baadhi ya wachezaji wao hawaitwi timu ya taifa kwakuwa hiyo ni hali ya kawaida
"Wachezaji wetu wanatoka kwenye nchi ambazo zina ushindani mkubwa na vipaji ni vingi kwahiyo kama hawajaitwa wakwetu mimi sioni kama ni ubaya, msingi ni kwamba kwetu wanaonyesha viwango vizuri, ni wachezaji wetu na wanajitahidi hiyo sioni kama ni ubaya," amesema Mwakalebela.
Aidha, Mwakalebela amesema kuitwa timu ya Taifa kwa wachezaji sio kipimo cha kujua mchezaji fulani ni mzuri ama la ila jambo la kuzingatia ni mchango wa mchezaji huyo awapo kiwanjani kutumikia kazi ya mwajiri wake kwenye Klabu.
"Kuitwa Timu ya Taifa inategemea na machaguo ya Mwalimu hata hapa nyumbani sisi tunaona tuna wachezaji wazuri tu wana mchango mkubwa katika vilabu vyao lakini hawaitwi timu ya taifa," hivyo kwetu kutoitwa kwa wachezaji wetu haitushtui''amesema Mwakalebela.
Itakumbukwa katika kujiandaa na msimu wa 2020-21 timu ya Yanga imefanya usajili mkubwa ulioleta gumzo mitandaoni kwakuwa timu hiyo kuongezeka kupitia usajili wa wachezaji wenye majina na viwango vikubwa barani Afrika.
Nyota wapya wa Yanga waliosajiliwa ni pamoja na Tonombe Mukoko na Tuisila Kisinda kutoka DRC Congo, Carlos Carmo Carlinhos kutoka Angola, Michael Sarpong kutoka Ghana, Yacouba Songne kutoka Ivory Coast, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya, Farid Mussa na wachezaji wengine wazawa.