Kocha wa Simba Sven Vandenbroeck (kushoto) na kocha wa Yanga Luc Aymael.
Sven ameyasema hayo leo kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa wao wamejipanga kucheza na kuchukua pointi ili mwisho wa siku watetee ubingwa wao.
“Tutacheza mchezo huu kama sio mchezo wa Ligi sababu kila mmoja anajua tumewaacha kwa alama kadhaa. Tutaucheza kama mchezo wa kweli wa wapinzani kwahiyo tunajiandaa kuchukua alama tatu na kusonga mbele ili mwisho wa msimu tushinde.” -Vandenbroeck.
Kwa upande wake nahodha wa Simba John Bocco amesema kuwa, “Sisi kama wachezaji tumejiadaa vizuri kwa mchezo wa kesho. Tunaahidi kwenda kucheza mchezo wa kujituma ili tuwafurahishe mashabiki wetu na ili tuweze kupata alama zote tatu”.