Kane na Grealish wamtesa Guardiola

Jumatano , 9th Jun , 2021

Klabu ya Manchester City wanampango wa kuongezea paund millioni 70 kwenye bajeti yao ya usajili kwa kuwauza baadhi ya wachezaji katika majira haya ya joto ili kusaidia harakati kubwa za kuwanasa nyota wawili wa England Harry Kane na Jack Grealis

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.

Kocha Pep Guardiola amesema kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji wasio na nafasi ya kucheza katika kikosi cha City kutaongeza pesa za uhamisho ili kutimiza malengo yake katika usajili.

Guardiola kocha bora wa msimu uliopita sasa anahitaji mshambuliaji wa kati kabla ya msimu mpya kuanza, na Harry Kane ndiye mchezaji chaguo la kwanza anayependekezwa na kocha huyo.