Beki wa klabu ya Juventus Giorgio Chiellini akishangilia moja ya bao aliloifungia klabu yake katika mechi za Seria A.
Bao la ushindi la Juve hapo Jana lilifungwa Dakika ya 66 na Beki wake Stephan Lichtsteiner ambae alikuwa Mchezaji wa Lazio kwa Misimu Mitatu kabla kuhamia Juventus.
Bao hilo la Juve lilitokana na Shuti la Simone Zaza kupiga Posti na Kipa Etrit Berisha kushindwa kuokoa Mpira uliorudi na Stephan Lichtsteiner kuuwahi na kuukwamisha wavuni.
Ushindi kwa juventus unakumbushia matokeo ya Fainali ya Coppa Italia Msimu uliopita ambapo walifanikiwa kuibwaga Lazio na kubeba Kombe.
Kibibi kizee cha Turin kilianza Msimu huu kwa kusuasua lakini sasa wameshinda Mechi zao 10 za Serie A, ambayo wao ndio Mabingwa Watetezi, na sasa wapo Nafasi ya Pili ikiwa ni nafasi murua kwao kwa kutwaa Taji lao la 5 mfululizo la Italy.
Kwenye Nusu Fainali ya Coppa Italia, Juve watawavaa Inter Milan, walio chini ya Kocha Roberto Mancini, ambao Juzi waliichapa Napoli 2-0 na kutinga Nusu Fainali.





