Wachezaji wa Simba
Mchezo huo wa pili kwa Simba, katika kundi B utapigwa saa 2:15 usiku ambapo Simba italazimika kusahihisha makosa yake ya ufungaji katika safu yake ya ushambuliaji ili iweze kupata ushindi mnono kama ilivyo kwa mahasimu wao Yanga.
Wakati Simba wakifikiria kupata ushindi katika mchezo leo, wapinzani wao KVZ nao wanataka kuitoa nishai timu hiyo inayoongoza ligi kuu Tanzania Bara kwani inalazimika kupata ushindi kutokana na kupoteza mchezo wake wa kwanza iliyopata kipigo cha 2-0 kutoka kwa URA.
Mechi nyingine inayopigwa hii leo ni kati ya URA na Jang'ombe Boys utakaopigwa saa 10 jioni, ambapo URA itaingia ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa 2-0 dhidi ya KVZ, wakati Jang'ombe Boys wakiingia huku wakiwa na majeraha ya kupigwa 1-0 na Taifa Jang'omba katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo.




