Mshambuliaji hatari wa Leicester City Jarmie Vardy ambaye atakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili katika moja ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza
Vardy, mwenye umri wa Miaka 28 ndie anaefungana na Romelu Lukaku kwa Ufungaji Mabao katika Ligi Kuu nchini Uingereza wote wakiwa na Magoli 15 kila mmoja.
Vardy ndie ameibeba Leicester City kuwa juu kwenye Ligi hiyo wakiwa Nafasi ya Pili na Pointi mbili nyuma ya Vinara Arsenal na Msimu huu huku akiweka Rekodi kwenye Ligi hiyo kwa kufunga Mabao katika Mechi 11 mfululizo.
Lakini tangu aweke Rekodi hiyo, Vardy amefunga Bao moja tu katika Mechi sita zilizopita Ukame ulioifanya Leicester ipokonywe uongozi wa Ligi baada ya kushindwa kufunga katika Mechi tatu na kuambua Pointi mbili tu kati ya hizo.

