Wachezaji Jannik Sinner na Matteo Arnaldi ndio walioipa kombe hilo Italia baada ya kushinda michezo ya fainali. Matteo Arnaldi ndio alijuwa wa kwanza kucheza na akashinda kwa seti 2-1 dhidi ya Alexei Popyrin wa Australia kwa seti 7-5, 2-6 na 6-4 na kuitanguliza Italia kuongoza 1-0 kabla ya Sinner kushinda dhidi ya Alex de Minaur kwa seti 2-0 yani 6-3 na 6-0.
Huu ni ubingwa wa pili wa Italia kwenye michuano hii n awa kwanza tangu mwaka 1976 hivyo huu ni ni ubingwa wao wa kwanza wa Davis baada ya miaka 47 kupita ngau walipochukua mara ya mwisho.