Alhamisi , 13th Jan , 2022

Klabu ya Inter Milan imefanikiwa kuwa Mabingwa wa Italian Super Cup kwa mwaka 2022 baada ya usiku wa kuamkia leo kuwafunga wapinzani wao Juventus mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Guisseppe Di Meazza, Italia.

(Wachezaji wa Inter Milan wakisheherekea Ubingwa wa Italian Super Cup)

Wawili hao walikutana kwenye mchezo huo baada ya Inter Milan kuibuka kuwa bingwa wa Serie A mwaka 2020-21 na Juventus kubeba kombe la Coppa Italia msimu huo.

Juventus ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kiungo wake Weston McKennie aliyefunga bao dakika 25 kabla ya Lautaro Martinez kuwasawazishia Inter dakika 35 ya mchezo na kulazimisha mchezo huo kuongezewa dakika 30.

Shujaa wa mchezo huo, aliibuka kuwa Alexis Sanchez aliyefunga bao kwenye dakika za nyongeza 120+1’ muda mchache sana kabla ya kuelekea kwenye changamoto ya mikwaju ya penalty kama mchezo huo ungesalia sare ya 1-1.

Ushindi huo umewafanya Inter Milan kuanza mwaka vema na kombe moja kabatini huku kocha wake, Simone Inzaghi akiweka rekodi ya kuwa kocha pekee kuifunga Juventus kwenye fainali nyingi zaidi tokea msimu wa mwaka 1929-30.

Na ushindi huo kwa Inzaghi umepatikana katika fainali tatu za Italian Super Cup, alipokuwa Lazio msimu uliopita na hivi sasa Inter Milan. Pia ni ubingwa huo ni wa 6 kwa Inter utofauti wa makombe 3 na bingwa wa Kihistoria  Juventus.

Alexis Sanchez ameweka rekodi ya kufunga bao la kwenye dakika za lala salama zaidi dakika 120+1’ kwenye Historia ya fainali za Italian Super Cup na kumpiku Gonzalo Higuain aliyefunga dakika 118 dhidi ya Juventus mwaka 2014.

Viita ya wawili hao kuwani amataji inaendelea kwenye Serie A ambapo Inter ni kinara akiwa na alama 49 utofauti wa alama 11 na Juventus aliyepo nafasi ya tano licha ya Inter kuwa nyuma kwa mchezo mmoja.