Jumatatu , 15th Jul , 2024

Bodi ya Wakurugenzi Simba SC imekubali maombi ya Ofisa Mtendaji Mkuu wao Imani Kajula ya kuachia ngazi ndani ya Simba SC kuanzia Agosti 31- 2024 huku klabu hiyo ikianza mchakato wa kutafuta Mtendaji Mkuu ndani ya wababe hao wa Msimbazi.

Kajula aliingia Simba mnamo Januari 2023 na kusaini kandarasi ya miezi 6 uliokuwa na kipengele cha kuongeza muda huku  alirithi mikoba ya Barbara Gonzalez aliyeondoka ndani ya Simba SC kipindi hicho.

Kajula anaondoka ndani ya Simba SC akishinda kombe la Muungano 2024 pamoja na Ngao ya Jamii msimu 2023-24,kufika hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika 2023-24 pamoja na kuanzisha mifumo bora ya Wanachama kama Simba Executive Network  kwa ajili ya kuiongezea mapato ndani ya klabu hiyo.
Utamkumbuka kwa lipi Imani Kajula ndani ya Simba SC?