Jumamosi , 1st Sep , 2018

Nyota wa Tottenham ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Korea ya Kusini Son Heung-min amefanikiwa kuepuka kwenda jeshini kwa miaka miwili baada ya timu yake ya taifa kuchukua ubingwa wa bara la Asia 'Asian Games' kwa kuifunga Japan mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

Mchezaji, Heung-min Son.

Katika mashindano hayo yaliyofanyika nchini Indonesia, Heung-min Son na timu yake ya taifa wameshinda ubingwa kwa mabao yaliyofungwa katika dakika za nyongeza baada ya kwenda sare dakika 90 za kwanza.

Son aliruhusiwa na klabu yake ya Spurs kushiriki michuano hiyo mikubwa barani Asia inayoshirikisha michezo mbalimbali.

Sheria za nchi ya Korea zinanawataka wanaume wote kuhudhuria mafunzo ya kijeshi ya nchi hiyo kabla hawajafikisha miaka 28 jambo ambalo,Son na wachezaji wenzake ambao wako chini ya umri huo wangelazimika kulitimiza endapo wangeshindwa kuiongoza timu yao kushinda ubingwa huo.

Son (26) alisajiliwa na Spurs mwaka 2015 kwa pauni 22 millioni kutoka klabu ya Bayer Leverkusen na kuisaidia klabu hiyo kumaliza nafasi nne bora za EPL katika misimu mitatu mfululizo ya mwisho.

Ameifungia klabu hiyo jumla ya mabao 47 katika michezo 140 aliyocheza mpaka sasa na ni mmoja ya wachezaji muhimu katika kikosi cha kocha Mauricio Pochettino.