Jumatatu , 20th Jun , 2016

Klabu ya Yanga imesema, hawawezi kuiomba Klabu ya Simba barua ili beki wao Hassan kessy aweze kupata ruhusa kutoka CAF kucheza mechi zilizobakia za hatua ya makundi ya FA Afrika.

Beki wa Yanga, Hassan Kessy

Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha klabu ya Yanga Jerry Muro amesema, walichokifanya Simba kushindwa kuwapa barua ili Kessy acheze katika mchezo wa jana dhidi ya Mo Bejaia ni kama kuwakomoa lakini wanaamini halitawezekana kwani njia zote wanazijua.

Muro amesema, vilabu vinatakiwa kuwa na uzalendo lakini kwa sasa wanaonyesha hakuna uzalendo na suala la Kessy kutokuwapa barua itakuwa sio uzalendo na watakuwa wanaendeleza ugomvu usiokuwa na maana.

Kessy iliwekewa kizuizi kuichezea Yanga katika mchezo wake wa kwanza hatua ya makundi shirikisho Afrika dhidi ya Mo Bejaia mpaka pale klabu ya Yanga itakapopata barua kutoka Simba na kuipeleka Shirikisho la soka barani Afrika CAF ili kuthibitisha kuwa Kessy ni mchezaji halali wa Yanga.