
Afisa Habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga amesema, mchezo wa kwanza utatoa sura ya timu nyingine na hata mwalimu atajua ni jinsi gani wachezaji watatakiwa kucheza ili kuweza kufanya vizuri katika michuano hiyo.
Maganga amesema, mchezo wa mpira ni mapambano hivyo hawawezi kuchagua watapambana na nani na watakaokutana nao ndio watakaocheza nao hivyo kinachotakiwa ni maandalizi na wanajiamini, kikosi kipo vizuri na tayari kwa kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.