Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa BFT, Wililo Lukelo amesema, mashindano hayo yalikuwa na changamoto nyingi kutokana na mabondia kucheza kwa kiwango cha juu hususani mabondia walio ndani ya Timu ya Taifa.
Lukelo amesema, kwa ujumla katika mashindano hayo wachezaji wa timu ya Taifa walionesha kiwango cha juu ambapo mpaka sasa hawajajua kama makocha watachagua wachezaji kwa ajili ya kuongezea katika kikosi cha timu ya taifa au kitabakia na wachezaji wale waliochaguliwa hapo awali ambao wanatarajiwa kushiriki mashindano ya All African Games.