Alhamisi , 12th Oct , 2023

Timu ya taifa ya Tanzania ya wasichana chini ya miaka 20 Tanzanite itacheza dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria kwenye michezo ya raundi ya tatu ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia kwa wasichana chini ya umri huo.

Tanzanite imefuzu raundi ya 3 baada ya kuitoa timu ya taifa ya Djibouti kwa ushindi wa jumla wa mabao 12-0 kwenye michezo miwili. Tanzanite imekata tiketi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 hapo jana kwenye mchezo wa mkondo wa pili mchezo uliochezwa Azam Complex Chamazi, baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 5-0. 

Kwenye raundi inayofuata Tanzanite itacheza dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria, na mshindi wa hatua hii atafuzu roundi ya 4 ambayo ndio ya mwisho kwenye hatua za kufuzu, washiundi wa raundi hii wanafuzu kucheza kombe la Dunia. 

Fainali za kombe la Dunia chini ya miaka 20 zitafanyika mwakani 2024 nchini Colombia na Afrika inapeleka timu 4 tu kwenye michuano hiyo.