Jumanne , 15th Nov , 2016

Kocha Gareth Southgate amesema bado hajaanza mazungumzo na Chama Cha Soka nchini Uingereza FA, juu ya kupewa mkataba wa moja kwa moja, kikiwa hii leo, anatarajiwa kumaliza mkataba wake wa mechi nne, kama kocha wa muda wa timu ya Taifa ya Uingereza.

Gareth Southgate

 

Kocha huyo, wa zamani wa kikosi cha Uingereza chini ya umri wa miaka 21, amepewa kibarua cha muda baada ya kufukuzwa kazi Sam Allardyce, aliyeiongoza timu hiyo kwa siku 67 pekee.

Southgate, amesema bado hajui kama atapewa kazi, lakini anaamini kabla ya mwezi huu kuisha, kila kitu kitajulikana, lakini vyanzo mbali mbali vya habari nchini Uingereza, vimedokeza kuwa FA ina mpango wa kumpa mkataba wa miaka 4, wenye thamani ya pauni milioni mbili kwa mwaka, na mazungumzo hayo, yanatarajiwa kuanza mara baada ya mchezo wa kirafiki, dhidi ya Hispania usiku wa leo katika Uwanja wa Wembley.