Jumapili , 9th Mei , 2021

Dereva wa magari yaendayo kasi, Lewis Hamilton ameendelea kuunguruma akitokea nyuma na kurudi dhidi ya mpinzani wake wa zamani Max Verstappen na kutwaa ushindi wa tano mfululizo huko Barcelona.

Dereva wa kampuni ya Marcedez, Lewis Hamilton akishangilia ushindi

Hamilton ameshinda Grand Prix ya Uhispania na kuongeza wigo katika safari yake ya ubingwa wa dunia juu ya Max Verstappen.

Max alijaribu kufanya ushujaa wa kumzuia Hamilton, lakini alishindwa kumpiku mpinzani wake mwanzoni mwa mapumziko mzunguko wa 60 na ule wa 66.

Hamilton alikua akitafuta ushindi wake wa tatu katika mashindano manne na kuongeza wigo wa alama kwenye Mashindano, huku Verstappen akishika nafasi ya pili na Valtteri Bottas akimaliza katika nafasi ya tatu.