Ijumaa , 21st Mei , 2021

Mlinzi wa Manchester United Harry Maguire ameongeza matumaini ya kwamba, huenda akawa fiti kwa fainali ya Ligi ya Uropa ya Manchester United dhidi ya Villa Real wiki ijayo baada ya kuonekana akitembea bila magongo jana usiku.

Mlinzi wa Manchester United, Harry Maguire akionekana kutembelea magongo.

Nahodha huyo wa Mashetani Wekundu amekuwa akifungwa kiatu maalum cha kumsadia na akitembea kwa magongo tangu alipopata jeraha la kifundo cha mguu dhidi ya Aston Villa mapema mwezi huu.

Lakini mlinzi huyo jana usiku alionekana akitembea bila visaidizi vyote alivyokua akitumua wakati alihudhuria hafla ya Sir Alex Ferguson pamoja na wachezaji wenzake pamoja na kocha Ole Gunnar Solskjaer, kitendo ambacho kinaleta matumaini kwa Man.united kwamba nahodha huyo anaweza akawa sehemu ya kikosi katika mchezo wa fainali ya Uropa.