Jumanne , 17th Mei , 2022

Afisa Habari wa Yanga Haji Manara amesema kuwa sare tatu mfululizo ambazo walizipata ziliwapa presha kidogo jambo ambalo liliweza kuwafanya wajipange kwa mara nyingine.

Afisa Habari wa Yanga Haji Manara

Kwenye mechi tatu ambazo ni dk 270 Yanga walikwama kushinda zaidi ya kuambulia sare mazima kwenye msako wa pointi 9 waliambulia pointi tatu.

Ilikuwa mbele ya Yanga, Ruvu Shooting na Tanzania Prisons ambapo kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Fiston Mayele alikosa penalti dakika  ya 38 na Heritier Makambo alikosa nafasi dk ya 88.

Manara amesema kuwa mpango mkubwa ambao upo kwa sasa ni kupata ushindi kwenye mechi zao ila haiwezi kuwa rahisi kutokana na kila timu kuwa kila timu inahitaji ushindi.

“Ilikuwa ni mwendo mbaya kwetu hasa ukizingatia kila kitu kipo na mbinu ambazo wachezaji wamekuwa wakipewa wanazitumia kusaka ushindi lakini matokeo yamekuwa tofauti.

“Ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuona tunakuwa kwenye mwendelezo mzuri kwani bado ligi inaendelea na hakuna ambaye amejihakikishia kuwa bingwa,” amesema Haji Manara

Yanga imekusanya pointi 60 ikiwa haijapoteza mchezo kwa msimu wa 2021/22,mchezo wake uliopita mbele ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma Yanga ilishinda mabao 2-0.