Alhamisi , 18th Jul , 2024

Mkufunzi Graham Potter amesema yupo tayari kurejea kwenye ukufunzi wa soka huku anahusishwa kurithi mikoba ya mkufunzi Gareth Southgate aliyejiuzuli nafasi yake ya kocha mkuu wa England kutokana na kupoteza kwenye fainali mbili za Euro 2020 na 2024 nchini Ujerumani.

Mkufunzi Graham Potter

Potter mwenye umr wa miaka 49 amesema kwa sasa nipo kwenye mazingira mazuri  na nina furaha ya kurejea kufanya kazi  ya ukocha na nipo tayari kwa ajili ya changamoto mpya pindi nikipata timu kwa sasa.

Mkufunzi Graham Potter aliyefukuzwa kazi ndani ya Chelsea mnamo Aprili 2023 amekuwa nje ya ukufunzi wa ukocha huku anahusishwa kuifundisha England sambamba na kocha wa Newcastle United Eddie Howe na kocha wa England chini ya Umri 21 Lee Carsley