Jumatano , 24th Jul , 2024

Shindano la wazi la mchezo wa Gofu"KCB East Africa Golf Tour" linatarajiwa kufanyika Agosti 3 katika Klabu ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania-JWTZ Lugalo Gofu Dar es Salaam.
-

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, leo Mwenyekiti wa klabu ya Gofu Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema, shindano hilo la siku moja limelenga kupata wachezaji wanne watakaoiwakilisha nchi kwenye michuano ya Afrika Mashariki itakayofanyika Kenya.
-
Alisema shindano hilo litakuwa la ndani na kuhimiza wachezaji wa Gofu waliopo Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha ili kujaribu bahati yao.
-
"Hili litakuwa ni shindano la kipekee litaka Sio hapa Tanzania watakwenda na nchi nyingine za Afrika Mashariki kufanya shindano kama hili na kutafuta wawakilishi watakaoenda fainali kule Kenya. Tunashukuru kwa kutudhamini,"amesema.

-
Alisema washindi wanne wa kila nchi watadhaminiwa kila kitu katika safari yao ya kuelekea kwenye fainali za Kenya.