Ijumaa , 16th Sep , 2022

Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Mathius Wandiba amesema hawatarajii kurudia makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanahitaji ushindi ili waweze kusonga hatua inayofuata.

Geita Gold wanatarajia kuwa wenyeji wa Hilal Alhasil ya Sudan kesho mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha bao 1-0 ugenini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Wandiba alisema wamefanyia kazi makosa waliyoyafanya mechi iliyopita wanatarajia mchezo mzuri na wa ushindani kutokana na ubora wa wapinzani wao.

“Wapinzani wetu ni wazuri na sisi ni bora pia tunatarajia ushindani mkubwa lani malengo yetu kama klabu ni kupata matokeo kwenye uwanja wetu wa nyumbani,” amesema Wandiba

Akizungumzia suala la kinara wa mabao, George Mpole ambaye alikosekana mechi iliyopita alisema anaendelea vizuri na amefanya mazoezi ya mwisho na timu suala la kucheza au kuto kucheza wao kama benchi la ufundi wataamua.

“Geita Gold kukosa matokeo kwenye mechi ya kwanza haina uhusiano wowote na kukosekana kwa Mpole kwani timu ina kikosi kipana lakini kurejea kwake itategemea na namna tutakavyopanga kikosi anaweza akachesa au asicheze.”