Jumamosi , 7th Sep , 2024

Taylor Fritz ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tenisi wa kwanza raia wa marekani upande wa wanaume kufuzu hatua ya fainali ya michuano ya Grand Slam baada ya kipindi cha miaka 15. Andy Roddick alikuwa mmarekani wa mwisho kufuzu hatua ya fainali kwenye Grand Slams mwaka 2009.

Taylor Fritz atacheza fainali ya michuano ya wazi ya tenisi ya Marekani (US Open) jumapili dhidi ya Jannik Sinner

Fritz amevunja rekodi hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya mmarekani mwenzio Frances Tiafoe kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya wazi ya marekani US Open mchezo uliochezwa kwa seti 5 yani 4-6, 7-5, 4-6, 6-4 na 6-1 mjini New York.

Na katika hatua ya fainali Taylor Fritz atacheza dhidi mchezaji namba kwa ubora Dunia Jannik Sinner mchezo utakaochezwa jumapili. Sinner amefuzu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa seti tatu mfululizo dhidi ya Mwingereza Jack Draper 7-5 7-6 na 6-2.