Jumanne , 24th Jul , 2018

Shirikisho la soka duniani FIFA limemwacha nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr kwenye orodha ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2018.

Mchezaji Neymar Jr kwenye tuzo za mwaka 2017.

Katika orodha ya majina 10 yaliyotajwa leo na FIFA nyota huyo hajajumuishwa, hali ambayo imezua mijadala mbalimbali kwa wadau wa soka wengine wakiunga mkono uamzi wa FIFA na wengine wakipinga kuwa alistahili kuwepo kwenye orodha hiyo.

Tuzo hiyo kwa msimu uliopita ilitwaa Cristiano Ronaldo na kuwashinda mpinzani wake Lionel Messi aliyeshika nafasi ya pili na Neymar Jr aliyeshika nafasi ya pili. Kwa upande wa makocha wa kiume tuzo hiyo alichukua Zinedine Zidane. 

Orodha ya wanaume

Cristiano Ronaldo - Juventus na Ureno
Kevin De Bruyne - Manchester City na Ubelgiji
Antoine Griezmann - Atletico Madrid na Ufaransa
Eden Hazard - Chelsea na Ubelgiji
Harry Kane - Tottenham na England
Kylian Mbappe - Paris St-Germain na Ufaransa
Lionel Messi - Barcelona na Argentina
Luka Modric - Real Madrid na Croatia
Mohamed Salah - Liverpool na Misri
Raphael Varane - Real Madrid na Ufaransa

Mchezaji Cristiano Ronaldo (kushoto) na kocha Zinedine Zidane (kulia) wakiwa na tuzo zao za mwaka 2017.

Orodha ya makocha wa kiume

Massimiliano Allegri (Ita) - Juventus
Stanislav Cherchesov (Rus) - Urusi
Zlatko Dalic (Cro) - Croatia 
Didier Deschamps (Fra) - Ufaransa 
Pep Guardiola (Spa) - Manchester City
Jurgen Klopp (Ger) - Liverpool
Roberto Martinez (Spa) - Ubelgiji
Diego Simeone (Arg) - Atletico Madrid
Gareth Southgate (Eng) - England 
Ernesto Valverde (Spa) - Barcelona
Zinedine Zidane (Fra) - Real Madrid

Orodha ya wanawake

Lucy Bronze - Lyon na England
Pernille Harder - Wolfsburg na Denmark
Ada Hegerberg - Lyon na Norway
Amandine Henry - Lyon na Ufaransa
Samantha Kerr - Perth Glory/Chicago Red Stars na Australia
Saki Kumagai - Lyon na Japan
Dzsenifer Marozsan - Lyon na Ujerumani
Marta - Orlando Pride na Brazil
Megan Rapinoe - Seattle Reign na Marekani
Wendie Renard - Lyon na Ufaransa

Orodha ya Makocha wanawake

Emma Hayes (Eng) - Chelsea 
Stephan Lerch (Ger) - VfL Wolfsburg
Mark Parsons (Eng) - Portland Thorns
Reynald Pedros (Fra) - Olympique Lyonnais
Alen Stajcic (Aus) - Australia 
Asako Takakura (Jpn) - Japan 
Vadao (Brz) - Brazil 
Jorge Vilda (Spa) - Hispania
Martina Voss-Tecklenburg (Ger) - Switzerland 
Sarina Wiegman (Ned) - Uholanzi