![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2023/08/08/fei.jpg?itok=2BsjHg92×tamp=1691505228)
Fei Toto amesema amejiandaa kukabiliana na viungo wa timu pinzani ili kuhakikisha wanaifunga Young Africans na kufuzu kucheza hatua ya Fainali ya Ngao ya Jamii.
“Malengo yangu makubwa katika msimu ujao ni kuipa makombe Azam FC, kwa kuanza tutaanza na Ngao ya Jamii kwani kombe hilo litatuongezea hamasa ya hali ya kujituma tuchukue bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu ujao''amesema Feitoto.
Ameongeza kuwa, anaheshimu ubora na usajili ambao Young Africans wameufanya katika kuelekea msimu ujao, lakini hiyo haimfanyi ahofie watakapokutana nao, kwa kushirikiana na wenzake anaamini watapata matokeo mazuri.
Kiungo huyo amejiunga na Azam FC katika usajili huu wa dirisha kubwa akitokea Young Africans.