
Michezo mitatau ya Euro 2020, kuchezwa leo
Timu ya taifa ya Italia ilianza vyema mashindano kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uturuki mchezo wa kundi A, ambao ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa michuano hii. Mabao ya Italia yalifungwa na Merih Demiral ambaye alijifunga, Ciro Immobile na Lorenzo Insigne.
Mchezo mwingine wa kundi hilo unachezwa leo Saa 10:00 Jioni, ambapo timu ya taifa ya Wales watakuwa wakiminyana na Switzerland, mchezo huu unachezwa katika dimba la Olympic mjini Baku nchini Azerbaijan.
Michezo mingine miwili itakayochezwa leo ni ya kundi B, Saa 1:00 Usiku mabingwa wa mwaka 1992 timu ya taifa ya Denmark wataonyeshana umwamba na Finland ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza michuano hii. Mchezo huu unachezwa Parken Copenhagen Denmark.
Mchezo wa mwisho leo utachezwa Saa 4:00 Usiku, moja ya timu inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa kwenye fainali hizi timu ya taifa ya Ubeligiji watkuwa wenyeji wa timu ya taifa ya Urusi. Mchezo huu utachezwa kwenye dimba la Gazprom, Saint Petersburg Urusi.