Jumapili , 13th Jun , 2021

Kiungo mchezeshaji wa timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen alianguka ghafla na kupoteza fahamu katika mchezo wao dhidi ya Finland kwenye mashindano ya EURO 2020 jumamosi hii tarehe 12/6/20221.

Wachezaji wa Denmark wakimkinga mwezao Christian Eriksen alipodondoka kiwanjani

Katika mchezo huo ambapo Finland aliibuka na ushindi wa bao 1-0 ,kiungo Christian Eriksen alianguka chini ghafla katika dakika ya 42 na kuzua taharuki kubwa miongoni mwa wachezaji na mashabiki walikuwepo uwanjani .

Waratibu wa mchezo walilazimika kuhairisha mchezo kwa dakika 52 na kisha kuendelea tena baada ya kujiridhisha Eriksen anaendelea vizuri huko hospitali alipokimbizwa

Hofu kubwa kwa sasa ni hatma yake kama anaweza kurejea tena kucheza soka,wengi wakikumbu kisa cha Fabrice Muamba wa Bolton Wonderers aliyelazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 23 baada ya kupata tatizo la moyo ghafla kwenye mechi dhidi ya Totternham 2012.

Eriksen kama atagundulika kuwa na tatizo la moyo, yawezekana akazuiliwa kucheza soka nchini Italia ambapo wanatumia kanuni hizo, kwa mujibu wa kiongozi wa juu wa idara ya afya NHS Dk Scott Murray

Naye nahodha wa Denmark Simon Kjaer anatajwa kuwa shujaa aliyeongoza mapambano ya kunusuru uhai wa Christean Eriksen kwa uweledi wa juu kwenye maeneo yote yaliyohusisha jambo hili pale uwanjani.

Katika mchezo mwingine Ubelgiji walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Urusi ambapo Roman Lukaku alifunga magoli mawili katika mchezo huo ambapo katika goli lake la kwanza alishangilia kwenye kamera na kusema’’ tunakupenda Chris’’ambaye ni mchezaji mwenzake wa Inter Milan.