Alhamisi , 31st Mar , 2022

Ligi kuu ya England inatarajia kuruhusu mfumo wa mabadiliko ya wachezaji watano katika mchezo mmoja kuanzia msimu ujao wa 2022/2023.

(Kibao cha kuonyesha namba za Mabadiliko ya wachezaji EPL )

Ikumbukwe tangu kutokea kwa athari za UVIKO 19 ambapo ligi zilisimama na baadae ziliporudi kuchezwa bila mashabiki, timu ziliruhusiwa kufanya mabadiliko ya wachezaji watano kwa muda, Kutokana na mrundikano wa michezo na kuvurugika kwa ratiba za ligi.

Lakini ligi kuu ya England wao walirudi kwenye utaratibu wa kawaida wa kufanya mabadiliko ya wachezaji watatu mwanzoni mwa msimu huu. Makocha kama Jurgen Klopp wa Liverpool na Pep Guardiola wa Manchester City walilalamikia suala hilo la kubadilisha wachezaji watano lakini walikutana na upinzani kutoka kwa makocha wa vilabu vidogo.

Imani kubwa iliyoko hivi sasa ni kwamba kwenye kikao cha kesho ijumaa cha Shirikisho linalotengeneza sheria za soka Duniani (IFAB) wengi wanaamini wataruhusu sheria ya mabadiliko ya wachezaji watano kuwa ndio utaratibu wa kudumu.