Wachezaji wa Barcelona na Real Madrid kwenye moja ya El Clasco katika uwanja wa Camp Nou
Mchezo huo maarufu kama El Clásico, unachezwa leo majira ya 5:00 usiku kwenye uwanja wa Camp Nou.
Huu ni utangulizi wa mechi nyingine kubwa 10 zitakazopigwa ndani ya mwezi Februari ikiwemo El Clásico ya marudiano itakayopigwa Februari 27.
LA LIGA
Mechi nyingine ni ile ya La Liga Februari 9 ikizikutanisha Atletico Madrid dhidi ya Real Madrid.
LIGI YA MABINGWA ULAYA
Mbali na hiyo kuna mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Manchester United dhidi ya PSG Februari 12.
Februari 13 pia kutakuwa na mchezo wa Uefa kati ya Borussia Dortmund na Tottenham.
LIGI KUU YA ENGLAND
Hapa Manchester United itakuwa mwenyeji wa Chelsea Februari 18 kwenye EPL.
LIGI YA MABINGWA ULAYA
Majogoo Liverpool watawaalika Bayern Munich, Februari 19.
Februari 20 Atletico Madrid watakipiga na Juventus.
LIGI KUU YA ENGLAND
Manchester United dhidi ya Liverpool itakuwa Februari 24.
Vijana wa Pep Guardiola Manchester City watakipiga na Chelsea Februari 24.
Februari ya kibabe itafungwa na mechi ya Chelsea dhidi ya Tottenham Hotspur tarehe 27.





.jpg?itok=5cvL0YaP)