Federer anayeshikilia nafasi ya tatu kwa viwango vya ubora duniani ametinga nusu fainali kwa kumshinda Tomas Berdyich kwa seti 7-6 (7-4) 6-2 6-4 .
Naye kinara kwa ubora duniani Djokovic ameendeleza harakati zake za kutaka kutetea taji lake baada ya leo kumshinda Kei Nishikori raia wa Japan kwa seti 6-3 6-2 6-4.
Mapema hii leo Serena William ambaye ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo upande wa wanawake ameshinda mchezo wake dhidi ya Maria Sharapova na kutinga nusu fainali.



