
Novak Djokovic ameshinda Wimbledon kwa mara ya 4 mfululizo
Katika mchezo huu wa fainali uliochezwa jana Julai 10, 2022 Djokovic alitoka nyuma baada ya kufungwa seti ya kwanza kwa 6-4, kabla ya kushinda set 3 mfululizo zilizofata kwa 6-3, 6-4 na 7-6. Hili ni taji la kwanza la Grand Slam kwa mwaka 2022 Novak Djokovic anashinda.
Huu ni ubingwa wa 4 mfululizo kwa Djokovic anatwaa kwenye michuano ya Wimbledon ameshinda kuanzia mwaka 2018, 2019, 2021 na 2022. Mwaka 2020 michuano hii haikufanyika kutokana na mlipuko wa Uviko 19, huu pia ni ubingwa wa 7 wa Wimbledon kwa Djokovic na hii ni Grands Slams yake ya 21 akiwa nyuma ya Rafael Nadal wa Hispania anayeongoza kwa kushinda mara nyingi akiwa na Grand Slam 22.
Baada ya ubingwa huu mchezaji huyo raia wa Serbia ambaye ni namba 7 kwa ubora Dunia amesema hatashiriki michuano ya wazi ya Marekani (US Open) kwa sababu hajapata chanjo ya Uviko 19. Masharti ya kucheza US Open kama sio raia wa Marekani basi ni lazima uwe umechanja au unamsamaa maalumu.
‘'sijachanjwa na sina mpango wa kupata chanjo kwa hivyo habari njema pekee ninazoweza kuwa nazo ni kama wataondoa sharti la kuingia bila kadi ya chanjo ya kijani iliyoidhinishwa au msamaha," Amesema Djokovic