
Mchezaji Hassan Dilunga (kushoto), Mohammed Issa Banka (Kulia)
Akizungumza na www.eatv.tv Kifaru amesema kuondokewa na wachezaji wake tegemeo, hawaogopi kwa kuwa wao ni chuo cha soka hvyo wanaanza kuunda upya kikosi chao kwa kuwatumia vijana walionao.
Kifaru amesema Mtibwa itawapasa kuandaa vijana wengine kama ilivyo sera yao ya kuwafua vijana na baadaye wanaimarika kama ilivyokuwa kwa Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim na wengineo.
"Tutatumia vijana tulionao kutokana na utamaduni wetu wa kuwafua vijana ambao huwa wanakuja kuwa na vipaji vizuri, kuondoka kwa Dilunga na Banka kwetu wala haitupi shida kubwa", amesema Kifaru.
Banka amefanikiwa kuchukuliwa na Yanga na kusainishwa mkataba wa miaka miwili pia Dilunga akitia kandarasi ya miaka miwili na Simba.