Alhamisi , 13th Jun , 2024

Klabu ya Coastal Union ipo mbioni kukataa ofa ya Simba SC juu ya huduma ya mlinzi wa kati Lameck Lawi

Simba walikuwa wanahitaji huduma ya beki huyo Kwenda kuimarisha eneo lao la ulinzi baada ya mkataba wa mlinzi wao raia wa DRC Henock Inonga kufikia tamati

Wekundu hao wa Msimbazi walitakiwa kutoa kiasi cha milioni mia tatu za kitanzania huku wakianza kutoa sehemu ya kiasi hiko ingawaje Coastal pia wanahitaji mchezaji huyo abaki kwaajili ya kuendelea kuwatumikia wagosi wa kaya ambao wamefuzu kucheza michuano ya shirikisho Afrika.

Lameck Lawi bado ana mkataba na Coastal Union hivyo kikosi hiko kitalazimika kuimarisha maslahi ya beki huyo aliyebeba tuzo ya mchezaji bora kijana msimu wa 2022-2023.

Mbali na Lawi Coast pia wamekataa ofa ya kumuuza mlinda mlango wao Matampi raia wa DRC ambaye ndiyo mlinda mlango bora wa ligi ya NBC 2023-2024