Jumatatu , 3rd Oct , 2016

Klabu ya Aston Villa ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Uingereza imemfuta kazi kocha wake, Roberto Di Matteo, baada ya kudumu kwa siku 124.

Roberto Di Matteo

Mchezaji huyo wa zamani na kocha wa Chelsea, aliteuliwa muda mfupi baada ya mfanyabiashara wa China, Dkt. Tony Xia, kuinunua klabu ya Villa katika mwezi wa Juni mwaka huu.

Villa sasa inatafuta mrithi wa Muitaliano huyo, ambaye anafukuzwa kwa matokeo mabovu ya kushinda mechi moja pekee kati ya 11 za ligi daraja la kwanza, Championship.

Steve Bruce na Mick McCarthy ndiyo makocha wanaotajwa kufaa kuchukua mikoba ya Di Matteo.