Jumapili , 26th Apr , 2015

Kwa mara ya kwanza hii leo jijini Dar es Salaam mashabiki wa michezo wameshuhudia mchezo wa aina yake kwa wachezaji mbalimbali kuchezea vyombo vya moto kwa mitindo na mbwembwe za aina yake nakukonga nyoyo za mashabiki waliokua wakishuhudia mchezo huo

Mmoja wa wachezaji wa mchezo wa kuchezea vyombo vya mto akichezea pikipiki

Mamia ya mashabiki wa michezo jijini Dar es Salaam hii leo walishuhudia burudani ya aina yake ya michezo ya kucheza na magari, pikipiki na viatu vya magurudumu michezo iliyofanyika katika viwanja vya leaders kinondoni

Wakiongea na muhtasari wa michezo mratibu wa tamasha hilo Siki Magoma na mwakilishi wa wadhamini wa tamasha hilo Silvester Joseph wamesema lengo kubwa lakufanya tamasha hilo ni kuitangaza na kuikuza michezo hiyo ambayo ni migeni hapa nchini na pia kutoa fulsa ya ajira kwa vijana

Aidha wadau hao wamesema mchezo wa kucheza na vyombo vya moto umekua maarufu sana barani ulaya, Asia na Amerika na umekua ni moja ya michezo ambayo unaziletea sifa kiurahisi nchi husika na pia kuzitambulisha nchi hizo kimataifa na ndio maana hata wao wakaona ni vema kuutambulisha rasmi hapa nchini japo kwa nyakati tofauti umekua ukichezwa na vijana mitaani kinyume na utaratibu na sasa wao wameutambulisha rasmi na kuanza mbio za kuutambulia wakianzia jijini Dar es salaam ambao zoezi hilo limeanza hii leo

Wakimalizia wadau hao wamesema pamoja na umuhimu wa mchezo huo lakini changamoto kubwa ni maeneo rasmi yakuchezea mchezo huo hasa ikizingatiwa mchezo huo ni mgeni hapa nchini na pia unahitaji eneo lenye nafasi ya kutosha kwa magari na pikipiki kuweza kuzunguka kiurahisi hivyo wanatoa wito kwa wadau kusaidia kuwekeza katika mchezo huo ili uweze kulitangaza vema taifa katika medani ya kimataifa.