CR7 “Sipo hapa kwa ajili ya Likizo”!

Ijumaa , 10th Sep , 2021

Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amefunguka na kusema hajajiunga na Manchester United kwa ajili ya likizo na badala yake amejiunga na miamba hiyo ya England ili kuendelea kubeba mataji.

Nyota wa Manchester United, Cristiano Ronaldo akiwa mazoezini Manchester United.

Ronaldo ameyasema hayo leo Septemba 10, 2021 akiwa anafanya mahojiano maalum na 'Manchester TV' na kujibia suala la uwezekano wa Manchester United kubeba mataji mbali mbali.

Ronaldo ameendelea kwa kusema; “Kipindi cha nyuma mambo yalikuwa mazuri, kushinda mataji mengi ya muhimu na kuvaa jezi ya Manchester United miaka mingi iliyopita lakini kwasasa nipo hapa ili nishinde mataji tena”.

“Ninauwezo huo mimi na wachezaji wenzangu. Nipo tayari kuanza safari hiyo. Ni nafasi nzuri kwangu, kwa mashabiki, kwa klabu kupiga hatua moja mbele”.

“Niko tayari na nafikiri na nitakuwa ongezeko kubwa sana miaka mitatu au minne ijayo”.

Ronaldo anataraji kushuka dimbani siku ya kesho Jumamosi Septemba 11, 2021 dhidi ya Newcastle United saa 11:00 Jioni kwenye uwanja wa St.James Park.

Michezo mingine itakayochezwa EPL Jumamosi ya kesho Septemba 11 ni Crystal Palace dhdi ya Tottenham Hotspurs 8:30 mchana, Arsenal na Norwich, Brentford itakipiga na Brighton Hove & Albion, Leicester City kuchuana na  Manchester City, Southampton itacheza na Westham United, Watford dhidi ya Wolves michezo hiyo mitano yote kuchezwa saa 11:00 Jioni ilhali  Chelsea vs Aston Villa saa 1:30 usiku.