
Philppe Coutinho akisaini mkataba mbele ya kocha wa Liverpool Jurgen Klopp
Taarifa zinasema Mbrazil huyo, amesaini mkataba utakaomuweka Anfield hadi mwaka 2022, huku kukiwa hakuna kipengele cha kumwachia mchezaji huyo.
Mara baada ya kusaini mkataba huo, Coutinho amesema kuwa anawashukuru watu wote wa Liverpool, na kuahidi kuitumikia klabu hiyo kwa nguvu zake zote, ili kulipa thamani anayopewa na klabu hiyo.
Coutinho aliyetoka kuuguza majeraha ya kifundo cha mguu kwa mwezi mmoja na nusu hadi sasa ameifungia klabu yake mabao 6, katika michezo 18, kwenye msimu huu.