Jumatatu , 2nd Jan , 2017

Straika wa Chelsea Diego Costa amesema alitaka kuondoka kwenye klabu hiyo katika msimu wa usajili uliopita.

Straika wa Chelsea Diego Costa

 

Costa alijiunga na klabu hiyo, maarufu kama Blues, kwa ada ya pauni milioni 32 mwaka 2014 na alikuwa amekaribia kurudi kwenye klabu yake ya zamani, Atletico Madrid, baada ya msimu mgumu wa 2015-2016 wa EPL.

Straika huyo amefunga magoli 14 katika EPL msimu huu na magoli yake yameisaidia Chelsea kuongoza ligi hiyo kwa pointi sita kufuatia klabu hiyo kushinda michezo 13 mfululizo.