Jumatatu , 19th Feb , 2018

Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Mzambia Obrey Chirwa amekanusha tetesi zinazosambaa kuwa anahitaji kiasi cha shilingi milioni 150 ili asaini mkataba mpya na Yanga.

''Sijawahi kusema wala kumwambia mtu yeyote kuwa nataka 150M kwa ajili ya mkataba mpya, sipendezwi na namna wanavyonizushia, nadhani nia yao ni kunigombanisha na wapenzi wa Yanga'', amesema Chirwa.

Aidha Chirwa ameongeza kuwa hapendezwi na maneno yanayoendelea mitandaoni kuwa amegoma kucheza wakati ukweli unajulikana kuwa ameumia na bado hajapona ndio mana hajasafiri na timu kwenda Shelisheli.

''Niliumia kwenye mchezo dhidi ya Majimaji ajabu wanasema nimegoma, mimi ni mchezaji wa Yanga, mimi na klabu ndiyo wenye kujua hatima yangu ya baadae, niacheni nicheze mpira"ameongeza.