Jumatano , 23rd Nov , 2016

Wenyeji Cameroon wameichapa Afrika Kusini bao moja kwa nunge na kufuzu kwa hatua ya nusu fainali ya Michuano ya AFCON kwa upande wa kina dada.

Mchezaji wa Cameroon - Ngo Mbeleck

 

Timu hiyo ya Cameroon ina uhakika wa kumaliza angalau katika nafasi ya pili katika kundi A, wakiwa wamesalia na mechi moja, wamepata alama sita kutokana na ushindi wao mara mbili.

Ngo Mbeleck, alifunga bao la pekee kunako katika dakika ya 83 katika mchezo huo uliochezwa mjini Yaounde, Cameroon, Jumanne.