Jumatatu , 6th Feb , 2017

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Cameroon Christian Bassogog ametangazwa kuwa mchezaji bora wa jumla wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON), iliyohitimishwa usiku wa jana kwa timu hiyo ya Cameroon kutwaa ubingwa.

Cameroon wakishangilia ubingwa

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaia 21, amelkuwa na mchango mkubwa katika mechi mbalimbali za mashindano ukiwemo mchezo wa fainali akiisadia Cameroon kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Misri katika dimba la Stade de l’Amitie mjini Libreville, Gabon

Aidha Benjamin MOUKANDJO pia wa Cameroon ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mchezo huo wa fainali huku tuzo ya timu yenye mchezo wa kiungwana (Fair Play) ikienda kwa Misri na mfungaji bora akiibuka Junior KABANANGA wa DR Congo aliyepachika mabao matatu katika michuano hiyo.

Kikosi bora cha mashindano kama kilivyotajwa na timu ya ufundi ya CAF ni kama ifuatavyo

Golikipa: Fabrice ONDOA (Cameroon)

Mabeki: Modou Kara MBODJI (Senegal), Ahmed HEGAZY (Egypt), Michael NGADEU (Cameroon)

Viungo: Charles KABORE (Burkina Faso), Daniel AMARTEY (Ghana), Bertrand TRAORE (Burkina Faso), Christian ATSU (Ghana), Mohamed SALAH (Egypt)

Washambuliaji: Christian BASSOGOG (Cameroon), Junior KABANANGA (DR Congo)

Katika michuano hiyo pamoja na Cameroon kutwaa ubingwa huo na kulipa kisasi imeondoka kwa rekodi ya aina yake ikiwemo kutoka mchezaji bora wa ujumla wa michuano hiyo lakini pia kutoa idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi cha mwaka cha Afrika.

Pia kocha mkuu wa timu hiyo ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza kutoka Ubelgiji kuweza kutwaa ubingwa wa Afrika.

Katika mchezo wa fainali Misri ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Mohamed Elneny katika dakika ya 22 kabla ya Cameroon kuchachamaa na kusawazisha bao lao katika dakika ya 59 mfungaji akiwa Nicholas Nkoulou kwa kichwa na Vicent Aboubakar akafunga bao safi ambalo liliipa ubingwa timu hiyo katika dakika ya 88 na kukamilisha ndoto ya Cameroon kubeba ubingwa huo kwa mara ya tano