Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kupimwa Afya yake ,Bondia Mwakinyo amesema kuwa amejiandaa vyema hakika itakuwa ni sikukuu ya Taifa hivyo mashabiki wake wajitokeze kwa wingi.
“Nilikaa nje kwa muda mrefu hivyo wapenzi wa ngumi watarajie kuona burudani ya aina yake kutok kwangu nimejiandaa kushinda “amesema Mwakinyo.
Kwa upande mwingine Bondia Mwakinyo ametoa Pongeza kwa Rais wa serikali ya Mapinduzji ya Zanzibar Dokta Hussein Mwinyi kwa kurudisha mchezo wa ngumi Visiwani Zanzibar.