
Viongozi wa Simba wakiwa kwenye kikao cha Bodi ya wakurugenzi wa timu hiyo.
Kwa mujibu wa Manara, pongezi hizo zimetolewa kwenye Kikao cha Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo kilichofanyika jana Januari 5, 2018 na kuongozwa na mwekezaji mkuu Mohammed Dewji pamoja na wajumbe wengine.
''Baada ya kikao cha bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika jana binafsi kikao kilinipa pongezi maalum kwa kuendelea kuitetea, kuisemea na kuilinda 'Image' na 'Brand' ya klabu hii kubwa kupita zote nchini'', amesema Manara.
Aidha Manara amesema moja ya jambo makhsusi kulijua kwa Wanasimba baada ya kikao cha bodi ya Wakurugenzi kilichofanyika jana, ni dhamira kubwa ya klabu kufanya vyema kwenye Ligi ya mabingwa Afrika na kutetea ubingwa wa ligi kuu.
Simba itaanza kampeni ya kuisaka robo fainali ya klabu bingwa Afrika kwa kucheza na JS Saoura kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Januari 12, 2019.
Mchezo huo ni wa kwanza kwa Simba katika kundi D lenye timu za Al Ahly ya Misri, Vita Club ya DR Congo pamoja na JS Saoura.